Tuesday, May 19, 2020

SMS za kumuomba msamaha mpenzi wako

Kugombana katika mahusiano ya kimapenzi ni sehemu ya mahusiano hivyo inapotokea kwamba mmegombana, basi unatukaiwa kumtumia meseji zifutazo ili aweze kukusamehe:

1. Hivi kweli haya ndiyo mapenzi ama naota njozi? Nimefanya kila naloweza kuliimarisha letu penzi lakini naishia kuambulia majonzi, nimekuwa mtu wa kububujikwa na machozi kwa sababu ya lako penzi, kama nimekukosea tafadhali niwie radhi mpenzi, nakupenda na amini wewe pekee ndiye uliyetimiza ndoto yangu ya mapenzi.

2. Hivi ni kosa gani nilililokutendea ambalo sipaswi kusamehewa? Ni kweli nilikosea nahitaji kusamehewa mpenzi, plz naomba nielewe kwani sina mwingine zaidi yako wewe. Luv u

3. Nakiri kweli nimekukosea naomba wako msamaha kwa yote yaliyotokea hakika nimekukwaza.

4. Lakini kwa hakika hii ni mara yangu ya kwanza naamini,naamini utanisamehe laaziz na kunipa nafasi ya kulienzi lako penzi.

5. Unajua nakupenda ila tu umeamua kunitenda rudisha moyo nyuma kisha twende sambamba mapenzi yanavyokwenda.

6. Mapenzi ni usanii ukiigiza utashindwa,mapenzi yanatoka moyoni wengi walioigiza walishatengana,mpenzi wangu usiniache.

7. Penzi la kweli siku zote hudumu,penzi la kitapeli haliishi ugomvi,mpenzi wangu leo nimegundua nakukosea na naahidi kubadilika na kuwa mpenzi mpya na bora,nisamehe .

8. Mpenzi nashukuru nikikuacha nitakuwa ninakufuru mi ndiyo mpenzio na hauna mwenzako mpenzi kuwa huru.

9. Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!

10. Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.

11.Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sina thamani katika hii dunia!

12. Kina ninapokukumbuka machozi yanidondoka, hivi leo mwana wa mwenzio ninaumbuka kwa kuparamia mapenzi kwa pupa, ukweli nakupa, hivi sasa najuta! Nisamehe mpenzi.

13. Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine katika moyo wako mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu mwanana....mwaaaaaaaa

Saturday, May 16, 2020

SMS ya kimahaba kumueleza mpenzi wako maana ya mapenzi, Mapenzi ni nini?

Mapenzi ni nini? Wale wasiopenda huita majukumu, wale
wanaoyachezea huita mchezo, wale wasiokuwa nayo huita
ndoto, na wale wanaoelewa huyaita mwisho wa safari, na
mimi, mwisho wangu ni wewe.

SMS nzuri kwa ajili ya kumtumia mpenzi wako kumwambia sababu ya kumpenda

mapenzi ni safari,mapenzi ni ahadi,mapenzi ni
ujasiri,mapenzi ni zawadi,mapenzi mitihani,mapenzi
ramani,mapenzi ajali na ndiyo maana nakupenda wewe bila kujali.

Ujumbe mzuri wa kumwambia mpenzi wako jinsi unavyompenda

sioni zawadi ya kukupatia kwa mapenzi
unayonipatia,
moyoni nimekuridhia wewe pekee penzi langu daima
kukupatia nakupenda

SMS ya kumtumia mpenzi wako kunapokuwa na wanafiki wanaoingilia penzi lenu

Wanafiki tusiwaombee kifo daima na milele washuhudie penzi
letu linavyozidi kukua,na tunavyopambana na mapito.

Ujumbe wa mahaba wa kumtumia umpendaye kumwambia anahisia gani kuhusu mapenzi

mapenzi ni hisia zilizopo moyoni mwetu,hujidhihirishe pale
unapopata umpendaye,utamu wake ni zaidi ya sukari uchungu
wake ni zaidi ya shubiri je kwako yapo je?

Friday, May 15, 2020

Meseji nzuri ya kumwambia mpenzi wako asichoke kukupenda

Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani
nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi
kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali
hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI

Meseji nzuri ya kimahaba ya kumtakia mpenzi wako usiku mwema

Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia,
fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu,
fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo
kwa kukutumia sms mpenzi wangu,
Nakutakia usiku mwema

Meseji ya kumkumbusha mpenzi wako kuwa unampenda

Mapenzi ni magumu na yatabaki kuwa hivyo, lakini kumbuka
kuna akupendaye naye ni MIMI!.

Meseji nzuri ya kumjalia hali umpendaye

USikimbie nyuki ukakosa asali, utamu wa samaki ni kula na
wali,
usizidishe siki akawa mkali.
Ni
mimi niliye na dhiki nakujulia tu hali.

Thursday, May 14, 2020

SMS ya ujumbe wa kimahaba wa kifumbo kwa mpenzi wako

Kila mtu anataka kuwa jua linalong’arisha maisha yako,
lakini ni afadhali niwe mwezi, ili nikuangazie wakati wa
giza ambapo jua limechwea na haliangazi tena.

SMS nzuri sana ya Kimahaba

Nimekuapata! Kama unanichukia, nipige mshale, lakini
tafadhali si moyoni sababu hapo ndipo wewe ulipo.

SMS ya kumshukuru mpenzi wako na kumwambia kuwa unampenda

nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua
furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu
nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu
tabibu ,we ndo wangu wa manani.


Ujumbe wa kumtumia mpenzi wako mlioachana kumwambia hakuwa sahihi

maumivu ya kulipoteza penzi lako ni kubwa, lakini ni
makubwa zaidi baada ya kugundua haukuwa yule nileyedhani.
inaniuma sana

Ujumbe wa kumwambia mpenzi wako kuwa utazidi kumpenda hata kama watasema mengi juu yake na juu ya mapenzi yenu

Hata kama watasema mengi kiasi gani, kwako wewe
nitaendelea kuwa mpole, maana nakupenda sana…

Ujumbe mzuri wa kumtumia mpenzi wako umpendaye sana

Lazima utakuwa mwizi sababu umeiba moyo wangu, umechoka
sababu unakimbia mara zote akilini mwangu, na labda mimi
sina shabaha sababu mara zote nikikulenga nakukosa.

SMS ya kumuonyesha mpenzi wako jinsi anavyokupagawisha

Watu waliniambia ninaweza kufanya chochote kama tu nitaweka mawazo yangu juu ya hicho kitu. Lakini kila nikijitahidi unaipoteza akili yangu

Friday, May 8, 2020

SMS ya kimahaba kwa mpenzi wako kumwambia unampenda sana hutaki hata sekunde ipite bila kumpenda

Good Morning Love SMS in English 250+ » Status Basket

"Kama mapenzi huweza kukimbiwa kwa kufumba macho yetu tu, basi nisingefunika macho kabisa. Sitaki sekunde ipite bila kukupenda wewe"

Meseji ya kumwambia mpenzi wako kuwa utampenda mpaka mwisho wa uhai wako



In a few words ❤️ Love Message, Love SMS & Poem - YouTube

"Penzi lako ndiyo pumzi yangu nawezaje kukuacha laazizi, ina maana nife??? Siwezi kukuacha nakupenda. Nitakupenda mpaka mwisho wa uhai wangu."

SMS nzuri ya salamu kwa mpenzi wako

I Love You Song | Kids Song | Love Song | The Kiboomers - YouTube

"Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu,
kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi"

Meseji nzuri ya kumtumia laazizi wako kumwambia jinsi unavyompenda

Love Messages: Best Heart Touching Romantic SMS | 143 Greeting

"Naukunjua moyo wangu huishi milele maishani ,nafungua nafsi nikupende wewe pekee,nafungmilango ya moyo wangu ili kutokupokea ugeni wowote wa moyo zaidi yako mpenzi.nakupenda sana laazizi"

SMS ya kumkumbusha mpenzi wako sifa za pendo la dhati

Red love - Clip Art Library

"Pendo la dhati lina sifa zifuatazo,kuvumilana, kusubiriana, kujaliana, kushauriana, na La Mwisho Ni Mimi Na Wewe"

SMS nzuri kuhusu maana ya mapenzi

Win a romantic luxury Valentines night in your own Penthouse ...

"Mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa unaempenda"

SMS ya kimahaba ya kumwambia mpenzi wako sababu ya kumpenda

Win a romantic luxury Valentines night in your own Penthouse ...

"wengi hupenda fanta kwa ladha yake,wengine hupenda pilipili kwa muwasho wake,wengine hupenda asali kwa utamu wake ila mimi nakupenda wewe kwa upendo wako."

Meseji nzuri ya kumuonyesha mpenzi wako jinsi gani umejitolea kwake

Win a romantic luxury Valentines night in your own Penthouse ...

Kama ungekuwa kidonda kwenye moyo wangu, ningekiacha na maumivu yake ndani yangu.

SMS nzuri ya kimahaba kumwambia mpenzi wako jinsi unavyotamani uwe naye kila sehemu na kila wakati

100+ Love Quotes with Beautiful Images | 121 Quotes

"Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali."